18 Aprili 2016 - 20:25
 Mwanamke aliyevaa hijabu atolewa katika ndege ya moja ya mashirika ya Kimarekani

Shirika mmoja la ndege la Kimarekani “Seuss West” lamshusha ndani ya ndege msafiri wake mmoja ambaye ni mwanamke aliyekuwa amevaa hijau, sababu ya kufanya kwao hivyo kunadaiwa kuwa ni kutopendezwa kwa mmoja kati ya wafanya kazi wa ndege hiyo kuhusu vazi lake la hijabu

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mwanamke mmoja muumini wa dini ya kiislamu aliyekuwa amevaa hijabu ameshushwa katika ndege ya shirika moja la Kimarekani la “Seuss West”.
Wasimamizi wa shirika hilo wametaja sababu ya tukio hilo ni kutokana na mfanyakazi mmoja wa shirika hilo kuto ridhishwa na vazi la kiislamu aliokuwa amevaa msafiri huyo.
Mwanamke huyo aliyekuwa na asili ya kutoka nchini Somalia ambaye kwa sasa anaishi katika jimbo la Maryland nchini Marekani, ametokewa na tukio hilo alipokuwa anasafiri kutoka “Chicago” kwenda “Seattle” nchini Marekani ndipo akakutana na mkasa kitu kilicho sababisha safari yake kuchelewa kwa masaa kadhaa.
“Hakimah Abdallah” alisema kuhusu suala hilo: awali ya yote mtumishi mmoja wa ndege hiyo alinitaka nibadili siti niliokuwa nimekaa na kwenda katika kiti kingine, lakini baada ya kuinuka kwangu katika kiti ndipo wakanichukua na kunitoa nje ya ndege.
Mume wa mwanamke huyo pia amesisitiza kwa kusema kuwa: kitendo cha shirika la ndege hio kufanya jambo hilo ni kwaajili ya kumdhalilisha mke wake kwakuwa yeye ni Muislamu na kuvaa kwake vazi la kislamu na hakuna sababu yeyote nyingine ya msingi.
Hii ni mara ya pili kwa shirika hilo kuwashusha abiria wake bila ya kutoa sababu za msingi, kwani wiki moja iliopita mtumishi wa shirika hilo alimshusha msafiri wa ndege wa shirika hilo kwakuwa alizungumza lugha ya kiarabu ndani ya ndege hiyo.

Hakimah Abdallah
mwisho wa Habari/290